Laana ni roho.

Kama pigo, haliachi mpaka limalize kuharibu waathirika wake. Ilizaliwa katika sehemu ambayo huwezi kutegemea kamwe.

Bustani ya Edeni ilikuwa kamili, paradiso ya kweli. Hakukuwa na njaa, ugonjwa, chuki au uovu wowote. Kifo hakikuwepo.

Kila kitu kilikuwa kitukufu, kikamilifu na maana ya kuwepo milele. Haki imeunganisha ushirika kati ya Muumba, uumbaji wake na asili..

Hata hivyo…

Kwa kutotii kwa mwanadamu, ufalme wa dhambi uliwekwa katika moyo wa mwanadamu.

Dhambi zote, japokuwa inaonekana haidhuru, ni kitendo cha uovu.

Inawezekanaje hakimu wa haki, ambaye kiti chake cha enzi kimeundwa juu ya usawa na haki, kuvumilia uovu?
Zaburi 97:2

Wasio haki walifukuzwa mara moja kwenye uwepo wake.

Ufalme wa wasio haki ulichukuwa nafasi ya ufalme wa haki katika moyo wa mwanadamu; Ufalme wa giza ulichukuwa nafasi ya ulimwengu wa nuru; Ufalme wa shetani ulichukuwa nafasi ya Ufalme wa Mungu; na laana ikachukuwa nafasi ya Baraka.

Na hivyo ubinadamu umekuja, tangu uasi wa wazazi wake wa kwanza.

Roho ya laana imepita kutoka kwa baba kwenda kwa mwana, kutoka kizazi hadi kizazi.

Dhamni ni laana.

Mwenye dhambi ni mtumwa wa laana.

Ili kuwekwa huru, mtumwa anatakiwa kuondoka au kuwekwa huru kutoka kwenye mkndamizo wake.

Hii ni sawa sawa na alivyofanya Ibrahimu.

Kujiweka huru yeye mwenyewe kutoka katika roho ya laana iliyoitawala nchi yake, familia yake na nyumba ya baba yake, Ibrahimu alitakiwa kuacha kila kitu.
Alijitenga na kila mtu ambaye angeweza kumshawishi kutotii sauti ya Mungu.

Alifanya dhabihu ya maisha yake ya dhambi.
Alijitoa katika laana ili awe Baraka yeye mwenyewe.

Vipi kuhusu , je wewe umekimbia laana ya dhambi?
Haiwezekani kuishi kwenye dhambi na kuwa Baraka.

Askofu Macedo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *