Kabla hatujaenda kazini kutokea nyumbani au kazini kwenda nyumbani , Mara zote huwa tunaacha maagizo na amri ambazo ni muhimu.

 

Kabla ya kupanda (kupaa), Bwana Yesu Aliamuru:

 

Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi… Mathayo 28:19

 

…Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

Marko 16:15

 

Kwa maneno mengine, ni juu yetu kwa kila mmoja wetu kutengeneza wanafunzi katika mataifa yote na kuihubiri injili kwa kila kiumbe.

 

Unadhani kulikuwa na chaguo wakati Bwana Yesu alipotoa amri hizi, lakini kwasababu alikuwa na vitu vyengine vingi , alisahau kusema ?

HAPANA! Mara millioni HAPANA!

 

Inawezakana kutengeneza wanafunzi popote duniani!

Inawezekana kwa Kanisa la Univeral kufika katika sehemu ambazo halijafika bado!

Yote hii inategemea kila mmoja wetu!

 

Kama mimi sio, wanafunzi hawatatengenezwa, na Injili haitahubiriwa kwa kila kiumbe.

 

Wewe, askofu, mchungaji, mchungaji msaidizi , shemazi… unasubiri nini?

 

Tunatakiwa kukuza ufalme wa Mungu hapa Duniani.

 

Bwana wetu anasema: Enendeni!

 

Kwahiyo twendeni sasa, hatuna muda wa kupoteza!

 

Askofu Macedo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *