Hakuna zaidi au pungufu yake.

 

Kinachookoa waliopotea ni IMANI katika Neno la Bwana Yesu Kristo;

 

Kinachorudisha maisha ni IMANI katika Neno la Bwana Yesu Kristo;

 

Kinachobadilisha maisha yaliyoharibika   ni IMANI katika Neno la Bwana Yesu Kristo!

 

Kinachomfanya mtu kuwa wa haki na thamani mbele za Mungu ni IMANI katika Neno la Bwana Yesu Kristo;

Kinachoponya ni IMANI katika Neno la Bwana Yesu Kristo.

 

Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamfatao. Waebrania 11:6

 

Kwahiyo , shaka lolote ambalo linaweza kuwepo tayari ni sababu ya hukumu, kwasababu ni dhambi. Hata wakati inapokuja kwenye chakula, kama kuna shaka katika unachokula, basi kuna dhambi (kuna hukumu). CHOCHOTE AMBACHO SIO KWA IMANI NI DHAMBI,

Hii ni mbaya. Tunahitimisha kwamba, chochote chenye mashaka ni cha shetani.

 

Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kama ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi. Warumi 14:23

 

Toa maoni kwa kifuatacho: Nani ataokolewa na imani?

 

Swali hili linajibiwa wakati mtu anapobatizwa na Roho ya Imani, Roho Mtakatifu.

 

 

Ni wale tu waliozaliwa kwa maji na Roho Mtakatifu wanaweza kuishi kutoka imani hadi imani na kwa imani. Hii ni kwasababu wale waliozaliwa na Roho ni Roho; hii ni kwamba wamezaliwa kwa Roho ya IMANI . N I wale tu ambao ni Roho (Imani) wana uwezo unaohitajika kuishi katika roho (katika Imani).

 

Mungu ni mwenye huruma kwetu kwamba kabla ya kutuagiza sisi kuishi kwa IMANI, Alitupa Roho wa IMANI kufanya iwezekane. Anawezaje atuamuru sisi kuishi katika imani na kwa imani kama kwanza hakutupa uwezo wa kufanya hivyo?

 

Tunapotangaza ubatizo wa Roho Mtakatifu, ni umuhimu wa kupata nguvu ya kuishi kwa imani na kutoka imani hadi imani, ukijua ya kwamba huwezi kumpendeza yeye na kuokolewa ukiwa na mashaka.

 

Imani ni uhakika kabisa; hakuna njia ya kuhisi imani…

 

Wakati kuna uhakika kabisa, kuna utiifu kwa Yule uliye na Imani naye.

Hii ina maana: imani + utiifu = miujiza

 

Askofu Macedo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *