Daudi alikuwa mtoto wa nane na wa mdogo zaidi wa Jesse, na kwahiyo akidharauliwa na baba yake mwenyewe. Kwasababu alikuwa bado mdogo, alichunga kondoo wakati kaka zake wakubwa walienda vitani

 

Lakini kijana huyu mdogo alikuwa wa IMANI, sana mpaka aliwashida dubu na simba, walipojaribu kuchukuwa kondoo katika kundi la baba yake. Daudi alijua kwamba hakuna chochote na yoyote anayeyeweza kufanya changamoto na Mungu wa Israel – haswa jitu lisilotailiwa Goliati .

Kwakua IMANI inatembea mkono kwa mkono na MAONO na UJASIRI, Daudi aliuliza nini kitafanyika kwa mtu ambaye atamshinda jitu .

Ahadi zilikuwa kama ifuatavyo:

 

  1. Mfalme atamtajirisha na utajiri mkubwa;
  2. Mfalme atampa mtoto wake ili amwoe
  3. Mfalme atawatenga nyumba ya baba yake na kodi katika Israel.

 

Ni hivyo !

 

Daudi alitengwa na baba yake na kaka zake, kwahiyo fikiria nini kilikuwa kinaendelea kwenye akili yake baada ya kusikia vitu hivi!

Alikuwa na maono ya jinsi gani maisha yake yatakuwa. Na alijua kwamba Mungu wa Israel hatamuacha. Hata hivyo, ilikuwa ni heshima ya Mungu mwenyewe iliyofanyiwa changamoto.

Kwahiyo kitu pekee kilichokosekana ni UJASIRI. Na Daudi alikuwa nazo nyingi!

Hakuhitaji silaha wala upanga kulishinda jitu lisilotahiliwa. Alichohitaji ni ujasiri wa kutenda.

Japo kuwa maisha yake yalikuwa hatarini, Daudi alimjua nani aliyemwamini.

 

Daudi akasema, “BWANA aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu ataniokoa na mkono wa mfilisti huyu. “ hakukuwa na njia ya Mfalme Sauli kumzuia. Na Sauli akamwambia Daudi” Enenda na BWANA atakuwa pamoja nawe.”

1Samweli 17:37

 

Kijana mdogo akachukua mawe matano kutoka kwenye kijito

-lakini, kiuwazi alihitaji moja tu.

Daudi alirusha jiwe, lakini Mungu ndiye alielielekeza kwenda katika paji la uso la jitu .

Kijana alietengwa matokeo yake amukuwa moja kati ya wafalme wakuu wa Israel.

Jiwe (Yesu) lililotumiwa na Daudi lilikuwa tayari katika kijito. Mtu yoyote angelirusha lile jiwe kwa Goliati.

Lakini IMANI, MAONO na UJASIRI wa Daudi umetoka wapi?

Kabla ya mapigano, Samuel alimtakasa yeye na roho wa Bwana akamjia Daudi.

 

Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho wa Bwana akamjilia Daudi. 1Samueli 16:13

 

Hii ndio sababu Mungu anatupa sisi Roho wake. Sio kwaajili ya kunena kwa lugha or kumsifu yeye , bali kuwa na IMANI, MAONO na UJASIRI kufanya matendo ya lazima

 

Askofu Macedo

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *