Yakobo alitakaswa kama mzaliwa wa kwanza wa baba yake Isaka;

Yakobo alikuwa na maono ya ngazi iliyojuu inayofika mbinguni;

Kwenye hayo maono , aliona malaika wakipanda na kushuka kwenye ngazi;

Yakobo alisikia sauti ya Bwana juu ya ngazi;

Yakobo alifanikiwa na akawa tajiri zaidi ya mkuu wake, Labani;

Yakobo mpaka wakati ule, alikuwa na watoto wa kiume 11;

Yakobo, tena , aliona jeshi la malaika ambao Mungu amewatuma kumuakikishia kuendelea kwa ulinzi.

Sababu gani Yakobo alikuwa nayo ya kumuhofia kaka yake?

Hofu ni ishara ya kuwa na hatia. Juu ya yote, kama huna cha kuficha, unakuwa huna cha kukufanya uwe na hofu.

Wakati mtu ambaye anakuwa ametiwa muhuri wa Roho Mtakatifu kwa kusudio akibeba roho ileile ya hofu na mahangaiko kama Yakobo, katika wakati huo, anakuwaa amepagawa na roho ya udanganyifu.

Anaweza kuwa na kuwa amefanikiwa kama Yakobo, lakini roho ya hofu haitamuacha peke yake mpaka asafishe dhamira yake mbaya mbele za Mungu.

Inawezekanaje mtu awe na Roho ya Mungu na roho ya hofu? Inawezekana kwa Roho Mtakatifu kuishi na roho ya hofu kwenye mwili huo huo?

Japokuwa Yakobo alikuwa na mtazamo wa KiMungu na kwa matokeo alifanikiwa, nafsi yake haikuwa na amani.

Kwa bahati mbaya, hii ni hali ya watu wengi “ waliobatizwa” na Roho Mtakatifu. Wanabeba roho ya hofu kwasababu wana dhambi ileile kama ya Yakobo: tabia mbaya.

Baada ya kujua kwamba Esau anakuja kukutana naye na wanaume 400.

” Yakobo akaogopa sana kufadhaika sana” Mwanzo 32 : 7

Kwahiyo akamlilia Bwana akisema: Yakobo akasema, “ Eee Mungu wa baba yangu Ibrahimu, na Mungu wa baba yangu Isaka, Bwana, uliyeniambia, Rudi uende mpaka nchi yako, na kwa jamaa zako nami nitakutendea mema. mimi sistahili hata kidogo hizo reheme zako na yote uliyomfanyia mtumwa wako maana nalivuka huo mto wa Yoridani na fimbo yangu na sasa nimekuwa matuo mawili, uniokoe sasa na mkono wa ndugu yangu, mkono wa Esau ,maana mimi namuogopa , asije akaja akanipiga , na mama pamoja na wana. Nawe ulisema, hakika nitakutendea mema na uzao wako nitaufanya kama mchanga wa bahari, usio hesabika kwa kuwa mwingi.” Mwanzo 32: 9 -12

Kilio

Kukata tamaa kwa Yakobo kulimfanya amlilie Mungu wa baba yake, wa Ibrahimu na Isaka . hiki kilio cha kukata tama hakikuhusisha hisia tupu , bali ilionyesha kuchukizwa na hali ile, na alisema : alikuwa Bwana aliyeniambia mimi nirudi kwenye ardhi yangu na kwa familia yangu na angefanya kila kitu sawa… hii ni sababu ya adhabu yangu kwa sababu ninatii neno lako. Nitaenda kukutana na hao wanaotaka kuniua na sina sharti la kukutana nao . ona hali yangu ! Kaka yangu anakuja na wanaume 400 kwa ajili ya vita. Nifanye nini?

Hata hivyo , hofu haikumuacha. Lakini Mungu alimpa muongozo: vina uzuri gani familia , utajiri , ahadi ya Mungu na haki ya mzaliwa , kama nikifa?

Kisha akatwaa baadhi ya vitu alivyonavyo, kuwa zawadi kwa Esau nduguye. Mwanzo 32 : 13

Ilikuwa ni yote aliyonayo kwa kubadilishana na maisha ya amani na kuwa mabali na hofu.

Zawadi ilikuwa na kondoo wakike 200, kondoo wakiume 20; ngamia 30 wa maziwa na wana wao na ng’ombe 10 ; punda 20 wa kike na wana wao 10 . hivi vilikuwa kwei vya thamani kwa mtu aliyeishi jagwani kwa wakati ule .

Akaondoka usiku ue akatwaa wakeze wawili , na vijakazi wake wawili na wanawe kumi na moja, akavuka kivuko cha Yaboki. Akatwaa , akawasha moto, akavusha na vyote alivyokuwa navyo. Mwanzo 32:22-23

Kutoka wakati huo, alibaki peke yake na bila ya chochote, akitegemea moja kwa moja Madhabahu .

 

Kwahiyo Malaika wa Bwana akamtokea yeye na kumbadilisha na akakiri : Nimeonana na Mungu uso kwa uso na nafsi yangu imeokoka. Mwanzo 32:30

 

Askofu Macedo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *