Nilikuwa natafakari juu ya matendo ya Roho Mtakatifu katika maisha ya wanadamu wa zamani. Katika Agano la Kale, kwa mfano. Mitume na mababu hawakuwa na Roho Mtakatifu wa kudumu pamoja nao kuwaongoza, walitegemea katika ndoto, ufunuo au sauti, kama ilivyokuwa kwa Nuhu, Abraham, Musa, Joshua n.k

Roho wa Mungu ilijithihirisha kwa kupitia watumishi wake, kuwapa mwelekeo na ilikuwa hivyo. Kisha watumishi walisubiria ufunuo mpya.

Sio kila mtu alikuwa na maono, ufunuo, au kusikia Sauti ya Mungu. Siku hizi tunaona matendo ya kudumu ya Roho Mtakatifu katika maisha ya wale wanaotamani kumfata Bwana Yesu. Alisema:

 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa msaidizi mwengine, ili akae nanyi hata milele… Yohana 14 : 16

Leo, hatuhitaji kusubiria ndoto, ufunuo, au kusikia Sauti yake ili kutuongoza. Hatuhitaji tena kulala usiku ili Mungu kutufunulia anachotaka. Hatuhitaji maono, kwasababu Mungu amepata njia ya kutuongoza sisi kwa kututumia Roho Mtakatifu.

Wale walio naye , wana ufunuo wa mapenzi yake , maono ya wokovu na wanaweza kusikia sauti ya Mungu mwenyewe kwenye Roho zao , wakishuhudia kuwa wao ni wake .

Wale wasio na Roho Mtakatifu wamepotea kabisa, hata kama wapo kanisani, machaguo yao, matendo, maamuzi na kushindwa ni matokeo ya machaguo yaliyofanyawa na mtu asiyeweza kusikia Sauti ya Mungu, anayeishi bila mwelekeo, kama kipofu.

Wale walio na Roho Mtakatifu wanaweza kuona mbali zaidi, hii haimaanishi kwamba Mungu anafanya maamuzi kwa ajili yetu , kwasababu japokuwa tunaye, anaheshimu mapenzi yetu, lakini anatuongoza sisi kwenye ukweli ili wale tu wanaotaka ndio waanguke.

Lakini yeye atakapokuja. Huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote… Yohana 16 : 13

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *