Mtumishi wa kweli, mzuri na mtumishi mwaminifu, anaweka mawazo yake yatazamie katika mapenzi ya Bwana wake. Na hii sio tu katika muda hadi muda, hapana! Ikiwa yupo kanisani, nyumbani, nje, hii ni kila mahali.

 

Siamini kwamba Mungu ana watumishi wa mara kwa mara. uwe ni mtumishi wake masaa 24 ya siku na siku 365 za mwaka, au usimtumikie yeye. Uwe ni Hekalu la Roho Mtakatifu, au sio.

 

Kwasababu hii, wale wanaomtumikia aliye Juu zaidi wanatambua majukumu yao na hawayaachi mbali nao kwa chochote. Familia , urafiki au majukumu yoyote kamwe hajataingilia katika kipaumbele cha kumtumikia Bwana. Muda wote anatawala mawazo ya mtumishi kwasababu yeye ni Bwana wake, Mmiliki wake , Baba yake.

 

Kilicho na utukufu zaidi katika mtumishi kwa Bwana ni msukumo wa mapenzi yake yanayotolewa na Roho Mtakatifu. Mtumishi hana mashaka kwa mapenzi ya Bwana; anajua nini anatakiwa kufanya na anafanya. Wakati huo huo, Bwana anasubiri mapenzi yake yatimizwe, na zaidi: haagizi yasiyowezekana. Anavyoagiza vyote unaweza kutoa au kufanya.

 

Pia mtumishi mzuri na mwaminifu anajua kumpendeza Bwana vizuri sana. Hii tunaona katika mfano wa watumishi watatu (Mathayo 25:14-30). Baada tu ya kukabidhi talanta, Bwana alisafiri. Walikuwa wanajua wanachotakiwa kufanya. Haina tofauti na sisi, kwasababu Roho wake yupo nasi.

 

Mtu akinitumikia na anifuate: nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamuheshimu. Yohana 12:26

 

Na Roho hutumikia zaidi kwa watumishi wake na kuamsha imani za wengine wote.

 

Askofu Macedo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *