Mungu mmoja,

Baba mmoja, Yesu Kristo mmoja, Roho Mtakatifu mmoja,

Bwana mmoja,

Imani moja

Familia moja,

 

Mwanamke mmoja, mwanamme mmoja,

Mume mmoja, mke mmoja,

Upendo mmoja…

 

Mlango moja,

Mdogo…

Barabara moja,

Nyembamba…

 

 

Uzima mmoja,

Katika ulimwengu huu na zaidi,

Paradiso au kuzimu,

Yerusalem mpya au ziwa la moto na kiberiti

 

Inategemea na uamuzi ya mmoja,

Sababu au moyo,

Hii inaleta tofauti,

Kati ya kuchaguliwa na kuitwa.

 

Kikombe cha Agano Jipya ni kimoja

Ni kikombe cha wokovu,

Washiriki wake wanakumbaliana wao kwa wao,

Kunywa damu yake katika Agano hili.

 

 

Hakuna omelet bila kupika mayai,

Hakuna wokovu bila imani ya dhabihu ,

Hakuna Agano bila dhabihu ya pande zote mbili,

Ya Muumba na alivyoviumba.

 

Ni ndoa gani inaishi bila ya wenza kujitoa?

Ni muungano gani unaishi bila ya dhabihu kwa wale wanaohusika?

 

Nani anaweza kunywa kutoka katika kikombe cha Agano jipya cha damu ya Yesu bila kutoa dhabihu binafsi?

 

Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana. 1 wakorintho 11:27

 

Kikombe cha wokovu ni kimoja; kinaashiria Yesu, Mzabibu wa kweli.

 

Wale wanaoshiriki wanakubaliana na Agano la Mungu Baba, katika njia ya matendo, kutoa sadaka mapenzi yao wenyewe.

 

Askofu Macedo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *