Mfungo wa Daniel unalingana na kusudi linaloelezewa katika sura ya 10 ya kitabu cha Daniel katika Biblia.

Kwa siku 21, Daniel aliamua kufunga kwaajili ya kutafuta kibali, busara na uelewa kutoka kwa Mungu. Siku hizi, kati ya vitu ambavyo mara nyingi huaribu ushirika na Mungu ni vikwazo – Aina zote za burudani na habari za kidunia ambazo hutupiga wakati wote.

 

Bwana Yesu alisema ”Mwenye masikio na asikie. Sababu ya kusema kwa Mifano”. (Mathayo 13:9). Hii ndio kusudi la mfungo wa Daniel: kufungua masikio yetu kwa sauti ya Mungu.

 

Kwahiyo, kati ya Januari 25 na Februari 14, tutaunganishwa na Mungu. Lakini nini kifanyike katika kipindi cha siku hizo?

 

Tafakari katika Neno la Mungu. Hii sio kuhusu kiwango cha kusoma, lakini ni kuhusu kitu gani unapata kutoka katika unachokisoma; Nenda kanisani katika kipindi hiki cha siku 21 kadiri unavyoweza kumtafuta Roho Mtakatifu; Kuwa na wakati wako na Mungu nje ya kanisa pia. Vipindi vya kusali. Kusali ni kuunganisha akili moja kwa moja na Mungu, nah ii inaweza kufanyika wakati wowote na sehemu yoyote.

 

Tafuta na kupata maudhui ya kiroho: katika Biblia, Blogu ya Askofu Macedo, Askofu Renato, na katika tovuti ya kanisa utakuta ujumbe wa kila siku.

Shiriki katika Mfungo wa Daniel ili Roho Mtakatifu aje katika maisha yako na kukufanya wewe Hekalu lake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *