Madhabahu ni sehemu ya Baraka , ushirika na ukaribu na Mungu . lakini pia ni sehemu ya dhabihu .
Ni kipaumbele kwa wale wanaoishi pale na kupanda maisha yao kwa ajili ya Roho ya Mungu ili wavune uzima wa milele kutoka kwenye Roho hiyo hiyo.
Chaguo la kutumikia Madhabahuni ni tukufu . sio rahisi . kinyume chake , kungekuwa na watumishi wengi .
Lakini ni Bwana pekee na watumishi wake wanaoweza kuhisi hii furaha ya utukufu wa matunda ya Madhabahuni. Wao ni wa milele kama dhahabu safi ; wenye heshima kama almasi…
Hakuna kitu chenye heshima zaidi ya kuwa kifaa cha Roho wa Mungu kwaajili ya wokovu wa nafsi.

Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? Mathayo 16: 26

Ukuu wote , utajiri na uzuri wa jua kuonekana duniani wakati wa mchana na mwezi na nyota usiku si kitu kulinganisha na utukufu wa wokovu wa nafsi moja.

Nafsi niya thamani sana .

Kama kungekuwa na nafsi moja tu imepotea kwenye hii dunia , Aliye Juu Zaidi angekuja kujifanya dhabihu yeye mwenyewe kwa ajili yake.
Haya ndiyo maono ya Mwenyezi kwa wanadamu ; na ni maono ya watoto wake pia.
Fikiria thawabu ya wale wanaookoa nafsi moja ! fikiria wale wanaookoa zaidi, Yeyote anayetaka kuhisi furaha ya muokoa nafsi anatakiwa aishi Madhabahuni na kupanda kwa Roho ya Madhabahu.

Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. Wagalatia 6: 8

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *