Kwanini upendo kama huo ?

Kwanini shauku kama huo ?

Ahadi na ahadi zaidi?

Nadhiri za upendo?

Uaminifu usioyumba !

Aliye juu zaidi huomboleza , hutamani na ana ndoto ya badiliko la wasiokuwa waaminifu na watu waasi kwenye taifa lake pendwa , Yakobo ambao watakuwa Israeli.

Mara ya pili nitakujenga, nawe utajengwa, Ee bikira wa Israeli mara ya pili utapambwa kwa matari yako, nawe utatokea katika michezo yao wanaofurahi. Yeremia 31: 4

Ni ajabu na kweli kuona Aliye juu anataka kusafisha kile ambacho hakuki chafua , kujenga kile ambacho hakuki bomoa, na kuona furaha kwa wale walio muudhunisha sana . kila wakati tunapotafakari neno la Mungu, tunapata nafasi ya kuona taswira ya tabia , njia zake za kuwa na jinsi ya kutenda katika hali tofauti . ni kama tunajenga mtu wake , karibia na yeye mbele za macho yetu.
Wakati wa kutafakari Yeremia 31, ninakiri nilitokwa na machozi katika macho yangu , kwasbabu sikuweza kufikiria na kumuona Mungu kama mtu , mtu anayeteseka kwasababu ya upendo , mtu aliyesalitiwa na kuchwa na kwa namna nyingine kusahaulika , lakini bado anauwezo wa kutamani sana ujio wa waliomsaliti na kupanga mipango yote ya furaha nautulivu kwa wale ambao kwa wale mara nyingi wamemkataa yeye , na haya yote bila chuki .

Unaweza kumfikirije mtu kama huyo ?

Tazamia na wewe utaweza !

Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu. Yeremia 31: 3

Ndiyo, Aliye Juu sana anaweza kuona wasaliti kama mabkira, hii ni, kwa walio safi na wasiyo safi. Anawaona kwa macho ya imani, Anatamani kwa upendo kuwasogeza kwake Mwenyewe.
Anaamini katika mabadiliko yetu!
Mungu amejaa mipango mema kwa kila mtu, lakini mipango hii inaweza kutimia tu katika maisha ya wale wanaoacha kutokuwa waaminifu (iwe kwa vitendo au madhumuni, kitu kilichofanyika aukuhisiwa tu ) na kupigana na nguvu zao zote kuwa, siku baada ya siku, mtu mpya, bikira wa kweli. Watu wa Israeli walifanya dhambi sana , na unaweza ukajiona mwenyewe kama MTENDA DHAMBI zaidi , lakini usisahau kwamba Mungu anakutamani ninyi, kama vile bwana harusi anavyomsubiri bibi harusi wake BIKRA

Mara ya pili nitakujenga, nawe utajengwa, Ee bikira wa Israeli mara ya pili utapambwa kwa matari yako……….

Kila wakati Mungu anasema, “atakuwa,” anasema kwamba kitu ambacho hakijawahi kutokea kitatokea (imani); mtu ambaye hajabadilika atabadilika!
Ruhusu Mungu awe Bwana wa nafsi yako. Je, unajua jinsi ya kufanya hivyo? Kuwa mtiifu wa KILA KITU kwa Aliye Juu, na hakika atakupenda kwa upendo wa milele.

Amina!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *