Alizeti hugeuka kulingana na sehemu yenye jua, kwa maneno mengine, “hufukuzia mwanga.”

Huenda tayari unajua jambo hili, lakini kuna ukweli mwingine ambao labda huujui!

Je! Umewahi kujiuliza ni nini kinachotokea kwenye siku za mawingu, mvua ,wakati jua linafunikwa kabisa na mawingu?

Hili ni swali la kuvutia, sivyo? Pengine unadhani hupukutika au hugeuza kichwa chake kuelekea chini. Je, hili ndio unaloliwaza akilini mwako ? Naam, hiyo si sahihi! Unajua kinachotokea? Wanageukiana kushirikiana nishati zao.

Ukamilifu wa asili ni wa kushangaza; sasa hebu tuweke hii kwenye maisha yetu.

Sisi sote tunataka hii nuru na kuitafuta kwa njia tofauti: katika familia zetu, marafiki, dini, kazi na kadhalika. Lakini kila wakati kunakuwa na siku za mawingu, siku za huzuni , kwa sababu hauwezi kuzikimbia! Wakati hii inatokea, watu wengi hujeruhiwa, huwa chini kiroho, na wale walio katika mazingira magumu zaidi, wakati mwingine, wanakuwa na masumbuko.

Asili ina mengi ya kutufundisha! ni kuhusu kufuata mfano wa maua ya alizeti? Katika wakati wa maumivu, kukata tamaa, maumivu, angalia ndani yako kwa uwazi na tambua pia kuna nuru ndani yako na hii nuru unaweza kuigawa na kwa wale unaowapenda.

Hisia ngumu na za maumivu ambazo zimesumbuliwa, hivi karibuni au baadaye, hugeuka kuwa ugonjwa. Je! Unahitaji kuathirika na ugonjwa ndo uanze kufanya kazi ya kuongea na wengine? Usifanye mambo kuwa magumu! Angalia alizeti! Haina kukaa juu, “O, jua limejificha, kwa hivyo nitasimama hapa nikijisikia huzuni, na kichwa changu nitashusha chini, nikisubiri lirudi..”

Hapana! Wakati huo huo, wao huamsha mwanga wao wa ndani na kugawana na wengine …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *