Maombi yana siri zake. Yanapaswa kufanywa chini ya masharti ya Muumba wake, sio muumbwaji.

Ana alifuata sala za mila kwa miaka mingi. Alienda Hekaluni mara kwa mara, akitoa maombi yake pamoja na sadaka ambayo mumewe alimpa – lakini kila kitu kilibaki vile vile mpaka:

Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba Bwana akalia sana. Akaweka nadhiri, akasema, “Ee Bwana wa majeshi” !

                                                                                                    1 Samweli 1.10-11

Katika maneno haya machache kuna siri kubwa ya maombi yenye ufanisi: lazima yawe na mwili, nafsi na roho!

KABLA : Ana alitoa sadaka ambayo mumewe alimpa; aliendelea kuwa na uchungu, huzuni, na kufikiri kwamba Mungu alikuwa amemfunga tumbo lake.

Lakini BAADA ya kutoa dhabihu yake mwenyewe, aliacha uchungu wake juu ya madhabahu, na akakataa kuamini kwamba kukosa kuzaa kwake ni mapenzi ya Mungu, alijibiwa!

Maombi yana siri zake.

Kwa imani na akili,

Askofu Macedo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *