Mara tu baada ya kubatizwa katika maji na kutiwa muhuri wa na Roho Mtakatifu, alimpeleka Yesu jangwani. Huko, alibatizwa kwa moto.

Kila Mkristo lazima kila mara aweke kwenye kumbumbu kwamba, kwa ujumla, matukio yote yaliyotokea katika maisha ya Bwana wetu pia yatatokea katika maisha ya mwanafunzi wake. Na huwezi kukimbia kutoka hapa. Baada ya yote, wale wanaofuata nyayo zake huwa tayari kukabiliana na miamba na miiba sawa na Yake … Japokuwa, hazina nguvu nyingi za kusababisha maumivu.

Wale ambao walitiwa muhuri  na Roho wa Mungu hivi karibuni, hawapaswi kushangazwa na ubatizo wa moto unaofanyika baada  tu ya huo, au hata huenda unapitia sasa hivi. Baki na furaha ndani kwa sababu hii ni ishara kwamba unapendwa.

Tafakari neno hili:

Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia.  1 Petro 4 :12-14

Nisamehe, lakini hivi sasa kuna mafuriko makubwa ya furaha kwangu.

Nami ninaweza tu kuelezea kama hii: hahhahahahahahaha

 

Askofu Macedo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *