VYOMBO   VITUPU 

Leo tunataka kuzungumza na wale ambao wana Roho Mtakatifu na wakati mfungo wa Danieli unakuja, unastaajabu: “Ikiwa nimewekwa muhuri tayari , kwa nini ninahitaji kufanya huu mfungo?”

Jibu ni rahisi na la moja kwa moja: kwa sababu ile ile ambayo mtu hawezi kuacha kuonyesha imani yake baada ya mafanikio makubwa, kwa kuwa Mungu wetu ni Chanzo cha uzima cha maisha na hufanyakazi kwa  nguvu zake kwa kipimo sawa  na tunachotumia  na ujasiri wetu!

Na ni nani kasema Kazi ya Roho Mtakatifu imekwamishwa na Ubatizo? Kwa nini hatuwezi kwenda zaidi katika ushirika wetu na Mungu ili kufikia uzoefu mpya na mkubwa zaidi, uvuvio,ufunuo, mawazo makuu, kwa sababu sio mambo yote haya pia kazi yake na faida ya kipekee kwa wale wanaomtafuta wakiwa na kiu? Utauelewa zaidi hii katika mazungumzo yafuatayo kati ya Mtume na mjane maskini.

Elisha akamwambia, Nikufanyie nini? Niambie; una kitu gani nyumbani? Akasema, Mimi mjakazi wako sina kitu nyumbani, ila chupa ya mafuta.  Akasema, Nenda, ukatake vyombo huko nje kwa jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usitake vichache.  Kisha uingie ndani, ukajifungie mlango wewe na wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo vilivyojaa ukavitenge.  Basi akamwacha, akajifungia mlango yeye na wanawe; hao wakamletea vile vyombo, na yeye akamimina.  Ikawa, vilipokwisha kujaa vile vyombo, akamwambia mwanawe, Niletee tena chombo. Akamwambia, Hakuna tena chombo. Mafuta yakakoma. “2 Wafalme 4: 2- 6

Kwa nini imeandikwa kuwa mafuta YALIKOMA badala ya KUISHA? Kwa sababu haiwezekani kwa kitu ambacho umepewa na   Mungu kiwe na kikomo au mwisho, wacha Roho Wake Mwenyewe! Mafuta yalikoma kwa sababu hakuwa na vyombo vingine vitupu, kama alivyofanya, angeweza kujaza vyote.

Bila shaka alitatua shida zake kwa kulipa madeni yake na kuishi katika ubora na wengine, lakini angeweza kwenda mbali.

Hali hiyo inatokea kwetu kuhusiana na Roho Mtakatifu, kwa sababu unapobatizwa, umekuwa umetatua tatizo lako la ndani, lakini pia unaweza kwenda mbali zaidi. Kama zaidi ukiishi katika ulimwengu huu, ikiwa tunajitolea kila siku mbele  ya Mungu kukabithi mapenzi yetu, miradi yetu binafsi, hisia zetu na matamanio, na kumtafuta kwa kiu, Kazi Yake katika maisha yetu hakika itapanuka zaidi ya ubatizo. Mambo makubwa bado yatakuja!

Mungu awabariki ninyi nyote!

Askofu Macedo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *