Imani na ujasiri hutembea mkono kwa mkono. Hakuna imani bila ya  ujasiri, kama vile hakuna ujasiri bila imani. Moja inategemea nyingine ili kupata mafanikio.

Mara tatu Mungu aliamuamuru Yoshua awe mwenye nguvu na mwenye ujasiri. Hakuwa akimaanisha nguvu za kimwili, lakini kwa nguvu ya kiroho, inayohusiana na imani ya kibinafsi.

Kila kitu katika maisha kinategemea imani na ujasiri. Imani ya kujiamini wewe mwenyewe na, juu ya yote, kwa Mungu, na ujasiri wa kuweka imani hii katika vitendo.

Imani inapaswa kutazamia uhusiano wa Mtu na Mungu. Awe na Imani kwake mwenyewe na kwa Mungu.

Wakati imani inalenga kwa Mungu tu, haifanyi kazi. Hii ndiyo kesi, kwa mfano, ya watu wa kidini. Wanajifunza kumuamini  Mungu, lakini sio wao wenyewe. Hii ndiyo sababu wanakosa nguvu zinazohitajika ili kuweka imani katika matendo. Kwa sababu hii, hawaoni matokeo ya matendo ya imani katika maisha yao ya kila siku.

Ingawa aliitwa, aliyechaguliwa na kutakaswa, Yoshua alipaswa kuzingatia mashauri ya Mungu ili kufanikiwa. Mungu alisisitiza mara tatu za mfululizo kwake awe mwenye nguvu na mwenye ujasiri, kwa sababu mafanikio yake yalitegemea hili. Musa alikuwa ameshamwambia kuhusu hilimwanzo . Naye Daudi akamwambia pia na  Sulemani (1 Wafalme 2 : 2).

Je! Ushauri huu umepoteza maana yake katika siku za leo? Mafanikio yoyote, ikiwa ni pamoja na Wokovu wa milele, unategemea ushauri huu ukiwekwa kwenye matendo .

Mungu ameamuru: nguvu na ujasiri. Kwa maneno mengine, kuwa hodari na mjasiri.

Mungu awabariki wote.

Askofu Macedo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *