Mungu amewapa mahitaji yote muhimu kwa watu wake ili kushinda Nchi ya Ahadi. Yeye ametupa Neno Lake, Roho Wake, na Jina Lake. Nini kingine tunachohitaji? Hakuna chochote kinachoshindikana kuptia vifaa hivi.

Kwa kweli, Neno Lake, Roho Wake, na Jina Lake havifanyi kazi bila ushirika wa wale wanaomwamini. Baada ya yote, sisi ni wafanyakazi wenzake wa Mungu. (1 Wakorintho 3.9)

Hiyo ni, Mungu hawezi kufanya chochote katika maisha yako bila ushirikiano wako! Hakuna maana ya kuomba wakati unapaswa kutenda! Musa hakuomba aliposimama mbele ya Bahari ya Shamu. Alipaza sauti ! Na jibu la Mungu lilikuwa: Kwa nini unalia kwangu? Waambie wana wa Israeli wasonge mbele! (Kutoka 14.15)

Labda umekuwa unaomba, kufunga na kumngojea Mungu kufanya kitu. Ikiwa ndio hivi, mpendwa wangu, sahau kuhusu kupokea jibu! Mungu kamwe hawezi kufanya sehemu yako, kama ilivyo vile wewe kamwe huwezi kufanya sehemu Yake!

Sisi ni washirika Wake. Na kila mmoja anapaswa kufanya sehemu yake ili muujiza uweze kutokea katika muungano huu!

Askofu Macedo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *