Jina la Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu yameingizwa katika Jina hili.

Bwana: Mungu Baba;

Yesu: Mungu Mwana na

Kristo: Mungu Roho Mtakatifu.

Sijui wala sina ufunuo juu ya siri iliyo nyuma ya Utatu Mtakatifu. Kwa imani, ninakubali kikamilifu, bila ya kivuli cha mashaka, kile Biblia inachonifundisha.

Japo kuwa, katika ubatizo wa Yesu tuna ufahamu kamili wa udhihirisho wa Utatu Mtakatifu: Mungu Mwana akibatizwa na Yohana Mbatizaji; Sauti kutoka mbinguni, akisema Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye, na hatimaye Mungu Roho Mtakatifu kwa njia ya njiwa akashuka juu ya Yesu. Mathayo 3:16-17

Je, unawaelezeaje watu watatu tofauti na Mungu mmoja?

Hakuna maelezo! Wale waliozaliwa na Roho Mtakatifu hawajali kuhusu kupata jibu kwa sababu wanajua kuwa vitu vya siri ni vya Bwana Mungu wetu, lakini mambo ambayo yamefunuliwa ni kwaajili ya sisi na watoto wetu milele … (Kumbukumbu la Torati 29:29)

Badala ya kusema, ” tu Baba,” tunaweza kusema kwa uhuru: “Mungu pekee.”

Kwa njia hii, tunamtazamia Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu.

Ubarikiwe katika Jina la Bwana Yesu Kristo!

Askofu Macedo

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *