Binti mdogo alifanya kosa na alipelekwa mahakamani. Adhabu ya makosa yake ilikuwa ni kufunwa maisha gerezani. Alilia akiomba msaada, lakini hakuna mtu aliyeweza kumsaidia. Wakati kesi hiyo ilipopelekwa mahakamani, alilia zaidi.

Familia na marafiki zake walimfuata, nao wakaanza kulia. Hakukuwa na tumaini. Hata hivyo, kuna kitu kilichotokea. Kabla ya binti huyo mdogo kukaa katika kiti cha utetezi, mtu mmoja alisimama na chumba cha mahakama kikakaa kimya. Kila mtu alimtazama. Alikuwa mtu mzuri na mwenye huruma. Naye akaingilia kwa ajili ya binti huyo.

Kesi ilikuwa ngumu, lakini alitumia nguvu zake zote, nishati na rasilimali kwa ajili ya kumpigania. Baada ya vita vya muda mrefu ya kisheria kati ya Yule mwanaume na washutumu wake, mwanamke huyo aliachiliwa. Alianguka kwa magoti mbele ya mtu huyo na akamwuliza, “Wewe ni nani?”

Siku iliyofuata, mwanamke huyo alifanya uhalifu mwingine kwa makusudi na alipelekwa kwenye mahakama ile ile .

Mara tu alipoingia, alimwona tena Yule mtu aliyemtetea jana , lakini wakati huu ameketi kiti cha hakimu. Hakuwa tena mwanasheria, sasa alikuwa hakimu. Kwa tabasamu juu ya uso wake, binti alisema, “Nipo hapa tena !”

Mtu huyo aliinua kichwa chake akasema, “Jana nilikuwa mwanasheria, kwa hiyo nilikutetea hata ulipokuwa na hatia. Lakini leo mimi ni hakimu na hukumu yangu lazima iwe ya haki. “

Kwa machozi machoni pake, aliuliza mara ya pili, “Wewe ni nani?”

Na huyo mtu akajibu, “Jana nilikuwa Mwokozi wako. Lakini sasa mimi ni hakimu wako. “

Leo, Yesu ni Mwanasheria wetu na Mkombozi, lakini siku itakuja ambapo Baba atatoa hukumu ya haki kwa wote.

YESU YUPO KARIBU, JIANDAE KUKUTANA NAYE !

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *