Hivi karibuni, mtangazaji maarufu wa televisheni alipanda ndege ambayo si sahihi na aligundua tu baada ya kutua katika jimbo lingine. Fikiria usumbufu na aibu aliyoipata.

Naam, maisha yetu hapa duniani ni ya muda mfupi. Nafsi zetu “zinasafiri” kwenda mwisho wa safari.

Ikiwa ulitakiwa kusafiri hadi seheu ya mbali sana leo, ungependa kuchagua usafiri wa aina gani? Ingekuwa kwa ndege, sio?

Na, inapokuja safari ya nafsi , kuna “viwanja vya ndege” viwili tu ambako zinaweza “kutua”: milele na Bwana Yesu au milele katika ziwa la moto na kiberiti.

Kufikia katika “uwanja wa ndege” wa Wokovu, tunapaswa kutumia IMANI INAYOOKOA, ambayo inatuongoza sisi kufanya dhabihu ya mapenzi yetu na tamaaa za dunia hii , ili kubaki imara katika njia sahihi.

Hii ndio imani ambayo huwafanya matowashi waepuke uovu wote ambao dunia hii unao, kama vile wale matowashi walijifanya wenyewe kwa Ufalme wa Mbinguni (Mathayo 19:12).

Hii ni imani muhimu zaidi. Ni muhimu kwa Wokovu wetu – hata kama safari imejaa vikwazo (kitu kisichowezekana kuepukika katika “safari” ya Ufalme wa Mbinguni).

Sasa, vipi ikiwa unaweza kuchagua daraja unalotsafiria ? Ungechagua uchumi, biashara au daraja la kwanza?

Bila shaka, ikiwa una hali ya kifedha nzuri , huwezi kusita kuchagua daraja la kwanza.

Ni sawa sawa na aina ya maisha unayokuwa nayo hapa duniani: inaweza kuwa maisha yenye Baraka katika kila eneo, na faraja yote ambayo ahadi za Mungu zinahakikisha, au la.

Hii itategemea IMANI YA KUTEKA . Inapatikana kwa kila mtu, lakini pia inahitaji dhabihu.

Wengi wako kwenye safari ya kwenda kwenye mwisho mbaya (kuzimu) – wengine katika daraja la uchumi (wanaishi kuzimu duniani), wengine ni katika daraja la kwanza (wanapokea baraka ambazo dunia hii zinatoa).

Wakati wengine wanaweza hata kuwa wasafiri kwenda sehemu sahihi (Ufalme wa Mbinguni), lakini wapo katika daraja la uchumi (bila kuchukua milki ya ahadi za Mungu).

Unachohitaji kufanya ni kusafiri kwenye mwisho sahihi (Ufalme wa Mbinguni) katika daraja la kwanza (pamoja na maisha ambayo yanamtukuza Mungu wako). Ili jambo hili lifanyike, vyote IMANI YA KUOKOA na IMANI YA KUTEKA ni muhimu.

Amini usiamini, safari tayari imeanza, na changamoto ya Israeli kwenye Mlima Karmeli ni hasa kwaajili ya hili.

Ikiwa uko kwenye ndege ambayo si sahihi, mara tu itakapo simama (na hii inahusu fursa ambazo Mungu anakupa), ushuke na uende kukimbilia ndege sahihi- iliyo kwaajili ya Ufalme wa Mungu. Kwa sababu hii, utahitaji Roho Mtakatifu zaidi ya vitu vingine vyote katika ulimwenguni huu.

Na kama uko tayari kwenye ndege sahihi (umetiwa muhuri na Roho Mtakatifu), sogea hadi daraja la kwanza. Unaweza kuwa na uhakika kuna nafasi inayopatikana, na hakuna mfanyakazi wa ndege katika dunia hii ambaye anaweza kukuzuia kusonga mbele huko!

Kumbuka tu, bila kujali chochote kinachotokea, jambo muhimu zaidi ni kufika mwisho wa mwisho!

Askofu Macedo

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *