Ni nani aliyemlazimisha Eliya kuwafanyia changamoto manabii wa Baali na kutoa sadaka juu ya Mlima Karmeli?

Ni nani aliyewahimiza watu ambao wamekuwa wakitoa ushuhuda kuweka kila kitu juu ya Madhabahu?

Waliisikia Sauti ya Mungu na walismua: kutii aukuto kutii.

Ikawa baada ya siku nyingi, neno la Bwana likamjia Eliya, katika mwaka wa tatu, kusema, Enenda, ukajionyeshe kwa Ahabu; nami nitaleta mvua juu ya nchi. 1 Wafalme 18.1

Mungu alimwambia Eliya tu ajionyeshe kwa Ahabu na kwamba ingekuwa mvua.

Lakini Eliya alitaka zaidi. kuchukizwa kwake dhidi ya kila kitu kilichokuwa kinatokea katika Israeli kulimlazimisha afanye changamoto, wazimu wa imani.

Ingekuwa vizuri kwa kila mtu ikawa mvua ingenyesha , hata hivyo, uharibifu wa kiroho, upofu, mgawanyiko wa imani, kila kitu kingeendelea kama ilivyokuwa.

Eliya alitaka zaidi!

Amri ilikuwa ni kwenda kwa Ahabu na kutangaza mvua.

Eliya akaenda kwa ajili ya yote au si kitu. Kwa sababu alitaka zaidi, alifanya zaidi!

Na Mungu, ambaye angeshusha chini baraka ya mvua, alijidhihirisha Mwenyewe kwa moto.

Ikiwa maisha yako hayakulazimishi changamoto, ni kwa sababu bado unaweza kuvumilia kidogo.

Changamoto ya Israeli ni kwa wale ambao wamechukizwa, wale ambao hawawezi tena kuvumilia , aibu, kudhalilishwa , kukata tamaa katika nafsi zao.

Ikiwa ni zaidi ya baraka zamvua, unataka Moto wa Roho Mtakatifu, kuchukua changamoto hii ya imani, yote au si kitu, maisha kwa maisha!

Wale ambao walikuwa hawaamini, wale ambao walikuwa kati ya mawazo mawili, walipoona moto, baada ya dhabihu na maombi ya Eliya, wakainama na kutambua kwamba Bwana ni Mungu Pekee wa Kweli.

Wale wanaokushutumu leo, wanaodhihaki imani yako na kukuita wewe wazimu, wataona moto wa Madhabahu na kusema: Bwana tu ndiye MUNGU!

Ameshirikiana na: Askofu Gonçalves

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *