Wale ambao wanaamini kuwa inawezekana kuwa Mkristo bila kufanya dhabihu wamekosea sana. Kuanzia Mwanzo hadi Ufunuo, dhabihu ni msingi wa maisha ya Kikristo na pia ni msingi wa kutembea na Mungu. Japokuwa, watu wengi wa kidini ambao mioyo yao imeweka juu ya dhahabu na sio Madhabahu hutumia vifungu vya bibilia nje ya muktadha kudhibitisha kwamba hatupaswi kutoa dhabihu. Lakini kila moja ya vifungu hivi, kwa muktadha wao sahihi, huongeza hitaji la kutoa dhabihu . Kwa mfano:

 

Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. . 1 Samweli 15.22

 

Je! Unajua ni kwanini Mungu anafurahishwa zaidi na utii kulikodhabihu ? Kwa sababu utii ni dhabihu ya kweli. Hakuna kitu kigumu kwa mwanadamu kufanya zaidi ya kukataa mapenzi yake. Inamuumiza zaidi kuliko kutoa kitu cha thamani.

 

Mapenzi ya mwanadamu ndiyo yanayo muongoza. Moyo humwonyesha njia ya kwenda, naye anaende. Yeye hutegemea mapenzi yake kufanya maamuzi. Watu wamezoea kuishi kwa matamanio yao hivi kwamba wengi hawawezi hata kufikiria kufanya vitu kwa jinsi ya tofauti.

 

Kutoa mapenzi yako na kufanya mapenzi ya Mungu ni kutambua kuwa anajua zaidi kuliko vile unavyoweza kujua.

Hakuna njia kwa Mungu kuwa Bwana wa mtu ambaye bado ni bwana wake mwenyewe. Hauwezi kutumikia mabwana wawili. Unapomtii Mungu,unakosa kujitii mwenyewe. Na unapojitii mwenyewe una kosa kumtii Mungu. Kile kinachomfurahisha Mungu huumiza moyo. Hakuna kati kati. Mungu hashirikiani kiti chake cha enzi na mtu yeyote.

 

Kwa sababu hii, dhabihu ni muhimu. Huondoa mapenzi yetu kutoka kwenye kiti cha enzi na inatoa udhibiti wa maisha yetu kwa Mungu. Dhabihu inaweka vitu katika nafasi yake. Kwa Kaisari vitu vya Kaisari. Kwa Mungu vitu ambavyo ni vya Mungu.

 

Unapotoa maisha yako kwa Mungu, unasalimisha kila kitu. Ikiwa bado haujasalimisha kila kitu, haujasalimisha maisha yako bado .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *