Tunajua kuwa bei ya bidhaa ikiwa juu, ndio kiwango chake huwa cha juu zaidi. Udhamini, uimara, umuhimu na ubora pia hujumuishwa kwenye bei. Wakati bidhaa ikiwa na bei ya chini, huwa tunashuku na kufikiria ikiwa inafaa kununuliwa. Tunaweza hata kuipeleka nyumbani, lakini tunajua kwamba mapema au baadaye tutahitaji kuibadilisha.

Kila kitu maishani kina bei yake – sio bidhaa za nyenzo tu lakini mafanikio ya kibinafsi pia. Na kile ulicho tayari kutoa kitaamua ubora wa kile utakacho kipata.

Je! utalipa shilingi ngapi kwa ajili ya ndoa yenye afya? Kwa taaluma iliyofanikiwa? Kwa afya? Kwa amani ya ndani?

Wengine wako tayari kutoa dhabihu haja za miili yao, wanatafuta mtu sahihi, na kufuata ushauri wa Mungu, wakati wengine wanapendelea kufanya wanachotaka, wanajitoa wenyewe kwa mtu wa kwanza anayekuja, na kufuata mioyo yao.

Wachache huwekeza katika kujifunza, kusoma na kufanya kazi kwa bidii. Wengi wanapendelea kudanganya mabosi wao, rushwa na kutembea juu ya watu wengine.

Wengine hufuata lishe bora na utaratibu wa mazoezi. Lakini watu wengi ni wavivu mno kufanya mazoezi na kila wakati wanakubali raha ya kula chakula kilicho na mafuta mengi.

Kati yetu, tuna wale ambao hufuata Neno la Mungu kwa uaminifu na wale wanaomfuata Bwana kwa njia zao wenyewe.

Hii ndio sababu kuna ndoa za kudumu na zilizoshindwa, taaluma zilizofanikiwa kwenye kurasa za majarida na wafanyabiashara wakubwa gerezani, watu wenye afya na wagonjwa, wanaoshinda katika imani na watu wa kidini wanaoteseka sana. Tofauti kati ya mmoja na mwingine iko katika bei ambayo kila mtu yuko tayari kulipa ili kufikia malengo yake.

Katika ulimwengu huu, ni rahisi kutumia uwongo kuliko ukweli ili kuteka, kwa sababu uwongo huleta matokeo ya haraka, na ukweli unahitaji wakati mwingi zaidi na nguvu. Japokuwa, usisahau: ugumu wa kupata mafanikio ni sawa na ubora wa mafanikio.Ikija haraka , itaondoka haraka.

Je! Uko tayari kulipa kiasi gani: gharama kubwa ya ukweli au gharama ya chini ya uwongo? Wewe ndiye unaye amua. Baadaye hautakuwa na haki ya kulalamika juu ya kile ulichorudi nacho nyumbani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *