BARAKA za leo ziongezwe katika maisha yako yote katika Jina la Mungu Mwenyezi.

Kidokezo cha leo ni juu ya FURAHA.

Wale ambao ni wa kidini, wenye kusaidia, wema, hawaishi katika dhambi, wako katika imani na waliobatizwa na Roho Mtakatifu, lakini WANALEA NDANI YAO ASILI , UBINAFSI, NA TAMAA MBAYA hiv karibuni au baadaye WATAANGUKA KWENYE MAJARIBU. Sijui kama wataweza kurudi…

Kwa upande mwingine, ingawa mwenye dhambi tena mbaya zaidi, anayetenda dhambi na kutumika kama chombo cha Shetani, bado ANAONEKANA NDANI YAKE, CHINI KABISA YA NAFSI YAKE ANA TAMANI KUACHA MAISHA ANAYOISHI NA KUISHI KWA HAKI, hivi karibuni au baadaye Mungu Mwenyezi. atampa nafasi ya KUANZA tena Maisha mapya.

Makundi haya mawili yanaonyesha NGUVU YA DHAMIRA ZA MOYO WA MTU, KWA WEMA au UOVU. Kila mtu anaweza kuchagua kwa uhuru. Kila mtu, KWA SABABU ZAKE, huchagua kwaajili yake yeye mwenyewe.

Hii ndio sababu Bwana Yesu alitabiri kwamba furaha ni kwa wale tu wenye njaa na kiu ya haki. Hii ni, hupewa wale ambao MAKUSUDIO YAO NI KUISHI KATIKA HAKI.

AMEHAKIKISHASHA KWAMBA WATAJAZWA NA FURAHA! Mathayo 5 : 6

 

Askofu Macedo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *