NILIJARIBU KUJIUWA MARA 3!

Haya yote yalikuwa ni uharibifu kwangu na nikawa nataka kujiuwa. Nilifanya jaribio la kutaka kujiuwa mara 3, lakini nilishindwa. Nikaanza kutafuta amani sehemu nyingine na hapo ndipo nikaanza kujihusisha na makundi yasiyo sahihi. “Marafiki” zangu walifundisha kunywa pombe na bila hata kutambua nikawa mlevi. Nilikuwa nakunywa kwa siri mbali ya wazazi wangu. Pia nikaanza kujiumiza, kupiga mwili, kuvuta sigara, kwenda kumbi za starehe na kuanza kijichora mwili. Nilikuwa nafanay vizuri sana katika masomo yangu, lakini hii haikunisimamisha mimi kuwa na chuki na mkali, badala yake nikaanza kupoteza mtazamo. Nilipigana na wavulana shuleni kwa sababu ya chuki niliyokuwa nayo kwa wanaume baada ya baba yangu kutuacha na kuanzisha familia nyingine. Kwasababu ya ulevi “nilipoteza heshima yangu”. Ikafika mahali ambapo nikachoka na kuwa furaha ya muda mfupi, sina kitu na nina mashaka. Mama yangu akanipeleka Kanisa la Universal ambapo nilijihusisha na Mnyororo wa maombi siku za Ijumaa kwaajili ya kupokea, Jumatano kwaajili wokovu wangu na Alhamis kwaajili ya familia yangu na nikaanza kuona nguvu ya mungu maishani mwangu. Leo mimi ni mwanamke tofauti. Nipo huru kutoka katika ulevi wote. Nimemsamehe baba yangu. Nina amani ya moyo na sitaki kufa tena kwasababu sasa najua Mungu yupo na ni juu ya vitu vyote.