Mungu alituma mapigo 10 kabla ya kuwatoa Israel kutoka Misri. Alimwambia Yoshua kuzunguka Yeriko mara 13. Alimponya Naamani alipooga mara 7 katika mto Yordani.  Nabii Elia aliomba mara 7 kabla ya kuona mvua inakuja duniani. Miujiza mikuu hutokea kila wakati ambao watu wanatii maagizo waliopewa na Mungu.

MNYORORO WA MAOMBI NI NINI?

Ni mwendelezo wa sala za wiki- wiki saba mfululizo- bila usumbufu kwa lengo la kufanikiwa kupitia imani. Kama ni uponyaji, mafanikio ya kifedha au mapokeo ya kiroho, Mnyororo wa Maombi utakusaidia kuendeleza Imani yako na kutambua jinsi ya kuyashinda tatizo lako.

KWANINI NATAKIWA KUJA ZAIDI YA MARA MOJA?

Kutokana na tatizo kuwa kubwa, baadhi ya watu huharibiwa na kuwa na wasiwasi ya kwamba kwanini ni ngumu kwao kutumia imani zao mara ya kwanza wanapohuzuria Ibada?. Bwana Yesu ametufundisha ya kwamba tusali siku zote na tusichoke (Luka 18:1).

Pale ambapo umeamua ni kitu gani unataka maishani, hatua inayofuata ni kujiuliza wewe mwenyewe: “Ni kwa jinsi gani nitaipata hiyo baraka?” jibu ni rahisi…

NINI NATAKIWA KUFANYA KABLA SIJAANZA?

Kabla hujaanza Mnyororo wa maombi, ongea na mchungaji kwa ushauri. Atakufundisha hatua kwa hatua jinsi ya kutumia imani yako kuyashinda matatizo yako. Usione aibu- neno moja la kukushauri linaweza kudhihirisha thamani, kuliko hata maombi wakati mwingine.

Fikiria Mnyororo wa Maombi kama tiba ya kidaktari. kama unavyokwenda kwa daktari na anakupima maendeleo yako kiafya, anakufatilia mpaka utakapo pona kabisa, nia yetu ni kuhakikisha kwamba unafaidika na Myororo wa Imani kwa kufanikisha baraka uliokuwa unaitafuta.

NATAKIWA KUJA MARA ZOTE SABA? ITAKUAJE NIKIKOSA SIKU MOJA?

Mnyororo wa maombi unategemea na uvumilivu wako. kama hautotumia uamuzi wako, haiwezi kufanya kazi. Pale utakapoanza Mnyororo wa maombi unajiingiza katika vita dhidi ya matatizo yako.

Mapepo mabaya yatajaribu kukusubirisha au kukuachisha kuendelea na Mnyororo wako, LAKINI CHOCHOTE KITAKACHOTOKEA, USIUVUNJE! chukulia kwa umakini na ushindi wako utapatikana.

INAFANYA KAZI KWELI?

Mnyororo wa maombi ni njia ya kibiblia ya kushinda baraka- na inafanya kazi kweli!

Imefanya kazi kwa watu wengi na itafanya kazi kwako. Haijalishi tatizo lako ni kubwa kiasi gani, Mnyororo wa maombi utakusaidia kulishinda. Tumia Imani yako, mpe Mungu ushahidi ya kujitoa kwako kwa Mnyororo wa maombi na utaona ni kwa jinsi gani Mungu atakutendea.