KAULI YA IMANI

Tunaamini:

  • Katika maandiko ya Agano Jipya na Agano la Kale katika asili ya maandiko kama ilivyohamasishwa na Mungu na kuyakubali kama makuu na mamlaka ya mwisho kwa imani na maisha. Katika Mungu mmoja, milele katika utatu-Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
  • Ya kwamba Yesu alitokana na Roho Mtakatifu, kazaliwa na Bikira Maria na ni Mungu kweli na Mwanadamu kweli.
  • Ya kwamba Mungu alimuumba mwanadamu katika mfano wake; kwamba mwanadamu alifanya dhambi kwahiyo atatumikia adhabu ya kifo, kimwili na kiroho; kwamba wanaadamu wote wanarithi dhambi ya asili ambayo inasababisha makosa kuhusiana na hatia ya kibinadamu
  • Ya kwamba Bwana Yesu alikufa kwaajili ya dhambi zetu, kama dhabihu kulingana na maandiko na kwamba atakaye mwamini wamethibitishwa juu ya misingi ya damu yake ambayo aliimwaga kwaajili yetu.
  • Katika kufufuka kwake Bwana Yesu, kupaa kwake kwenda mbinguni na uwepo wake katika maisha kama kuhani mkuu na wakili wetu.
  • Katika kurudi kwa Bwana Yesu katika Utukufu.
  • Ya kwamba wale wanaotubu dhambi zao, wanampokea Bwana Yesu Kristo kwa imani, wamezaliwa tena na Roho Mtakatifu na kuwa watoto wa Mungu.
  • Katika ubatizo wa Roho Mtakatifu ambao huwezesha waumini kwaajili ya huduma, pamoja na kuandamana na zawadi zisizo za kawaida za Roho Mtakatifu na katika ushirika wa Roho mtakatifu.
  • Katika Mungu ameweka huduma za mtume, nabii, mhubiri, mchungaji na mwalimu.
  • Katika ufufuo wa wenye haki na wasio haki, baraka za milele za waliokombolewa, na kutupwa kwa wale walioukataa wokovu.
  • Ya kwamba Kanisa la ukweli linaambatana na wale wote waliokombolewa na Yesu Kristo na wale waliozaliwa upya na Roho Mtakatifu; na kanisa la duniani linatakiwa lichukuwe tabia kutoka katika dhana ya kanisa la kiroho na hivyo kuzaliwa upya na kutubu ni muhimu kwa waumini wa kanisa.
  • Ya kwamba Bwana Yesu Kristo amechagua kanuni mbili- ubatizo wa maji na mlo wa Bwana; yaonekane kama matendo ya utii na kuendeleza ushuhuda kwa ukweli wa imani ya Kikristo; ya kwamba ubatizo ni kuzamishwa katika maji kama kutubu kwa Bwana Yesu katika kuzikwa na ufufuo na ya kwamba chakula cha bwana ni kushiriki mwili na damu ya Mwokozi wetu katika kukumbuka Dhabihu yake mpaka atakapokuja.
  • Ya kwamba uponyaji wa Mungu katika Agano la kale na Agano jipya ni sehemu ya Injili.
  • Biblia inafundisha ya kwamba bila utakatifu, hakuna atakayemwona Mungu.
 •  Katika utakaso kama ufafanuzi, bado mwendelezo wa kazi ya neema, kuanza katika wakati wa kuzaliwa upya na kuendelea mpaka mwisho wa maisha.