1. Skip to Menu
  2. Skip to Content
  3. Skip to Footer>

Family Life Testimonies

PDF Print E-mail

  
Felista Raymond Tarimo

Nilikuwa mlevi zaidi ya miaka 10. Hali hii ilikuwa ikiharibu Familia yangu, watoto wangu and muonekano wangu.

Familia yangu ilikuwa ikinitegemea, kwa ajili ya Elimu, kuwapatia chakula na mavazi, lakini kila shilingi niliyoipata nilitumia kunywa pombe. Ili fika kipindi nilichoka aina ya maisha niliyokuwa nikuishi, kwa hiyo nikaenda kwa waganga kutafuta msaada; walinipa kila aina ya miti shamba ili niweze kuacha kunywa pombe lakini haikusaidia kitu.

Siku moja nilikaribishwa kuja katika Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu na nikaenda kanisani nikazungumza na Mchungaji nikamwambia kuhusu matatizo yangu, Mchungaji akaniambia kwamba maisha yangu yanaweza kubadilika. Akanishauri kuhusu mnyororo wa maombi wa Ijumaa saa 11:30jioni na Jumapili saa 4:00asubuhi.

Nilifuatilia mnyororo wa maombi kama ilivyoongozwa na nikapona mabadiliko maishani mwangu; Leo nipo huru kutoka kwenye ulevi wote, naweza kutunza familia yangu na matatizo niliyokuwa nayo mwanzoni sasa yameondoka yote. Hatimaye nipo huru!


 

 

Today's Quote

“Faith is not the belief that God will do what you want. It is the belief that God will do what is right.”

Max Lucado

Weekly Messages


Name:

Email: